Sunday, November 4, 2012

MASTER PARADE

 
                                                         Tukiwa Parade siku za Jumatatu

Saturday, November 3, 2012

UJUMUISHO WA MATUKIO Oct 2012..

Uzinduzi wa G H T ( Galanos House of Talent) uliifanya tarehe 27/10/2010 kuwa nzuri ikiambatana na Mabadiliko ya Ratiba ya chakula ambayo wanafunzi wametokea kujivunia na kufurahia...

MATOKEO YA MOCK..
Matokeo ya mtihani wa kujipima wa Kanda yaani Mock yameshuka kwa kiwango kikubwa sana hususani katika somo la HESABU/ADV.MATHEMATICS ambayo hayakua ya kuridhisha sana..
Kanda nzima A=O, B=1, C=2, D= kadhaa ikifuatiwa na E,S na F.. Wanafunzi pamoja na waalimu wamejadili na kubaini tatizo na kuapa vikali kwamba mabadiliko yata fanyika NECTA....

Monday, July 9, 2012

SERIKALI YA WANAFUNZI GALANOS 2012-13

Waalimu wametilia mkazo juu ya Serikali mpya ya Wanafunzi kwa kuogopa viongozi wasio bora... Hii imeoneshwa wazi baada ya vikao mbalimbali kufanyika na majadiliano ana kwa ana na Viongozi wastaafu ili waweze kutambua nani anaefaa kuchukua fomu za maombi, aidha uchaguzi huo ambao utafanyika wiki ijayo umejumuishwa na usimamizi mkali juu ya waombaji hao kwa kuzingatia sera zenye maadili zisizo na kashfa wala matusi kwa Waalimu au Serikali kwa ujumla.....